Waziri Mkuu Majaliwa ameyasema hayo wakati akizungumza na watumishi na Madiwani wa Halmashauri ya wilaya ya Tandahimba mkoani humo ambapo amesema ni lazima viongozi hao wasimamie nidhamu kwa kuwalinda watoto wa kike katika wilaya hiyo wasipate mimba ili waendelee na masomo.
"Hawa mabinti wote wamepotea, wamepoteza muelekeo. Nataka kuona mabadiliko mwaka huu 2018 hatutaki kusikia tuhuma, matatizo ya wanafunzi wetu kuacha shule kwa sababu ya mimba. Hawa vijana wote wanaohusika kuwapa mimba wanafunzi ni kuwakamata na kuwapeleka jela bila ya huruma", amesema Majaliwa.
Msikilize hapa chini Waziri Mkuu Majaliwa akiongea mengine zaidi.





