Jumatatu , 21st Sep , 2020

Kiungo wa zamanai wa FC Barcelona, Arsenal, Chelsea na timu ya taifa ya Hispania Cesc Fabregas amesema Sadio Mane Ndio mchezaji bora kwenye ligi kuu England EPL.

Sadio Mane alijiunga na Liverpool mwaka 2016 akitokea Southampton

Mshambuliaji huyo wa kimataifa wa Senegal aliifungia timu yake ya Liverpool mabao mawili kwenye mchezo wa ligi kuu England EPL dhidi ya Chelsea mchezo amabao Liverpool walishinda kwa mabao 2-0 mchezo uliochezwa katika dimba la Stanford Bridge.

Licha ya kufunga mabao hayo mawili Mane alikuwa kwenye kiwango bora sana katika mchezo huo, na huu ni muendelezo wa kiwango bora cha uchezaji kwa mchezaji huyo kwani tangu ajiunge na kikosi cha Liverpool mwaka 2016 akitokea Southampton amekuwa moja ya wachezaji muhimu kwenye kikosi cha kocha Jurgen Klopp.
 

Cesc Fabregas ambae kwa sasa anaichezea klabu ya Monaco ya Ufaransa ameandika kupitia ukurasa wake wa tweeter "nitasema tena. Sadio Mane ni mchezaji bora kwenye ligi'

Unaweza ukasema Fabrega ni shabiki mkubwa wa Sadio Mane kwani mwezi oktoba mwaka 2019 kupitia ukurasa wake wa tweeter aliandika kuwa Mane ni miongoni mwa wachezaji watatu bora duniani.

Mane mwenye umri wa miaka 28 huu ni msimu wake wa tano akiwa na kikosi cha Liverpool na amecheza jumla ya michezo 173 amefunga mabao 83 katika michuano yote na ameshinda mataji manne ukiwemo ubingwa wa klabu bingwa ulaya na ubingwa wa ligi kuu England EPL.

Kauli hii ya Fabregas imezua mjadala mkubwa miongoni mwa mashabiki na wadau wa ligi kuu England kwani kuna wanao amini kiungo wa Manchester City Kevin De Bruyne.