Jumanne , 23rd Aug , 2022

Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge na Uratibu George Simbachawene, amemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan kwa kutoa kiasi cha shilingi billioni 16 kwa mwaka uliopita wa fedha ambazo zimetekeleza miradi mbalimbali katika Halmashauri ya Mpwapwa.

Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge na Uratibu George Simbachawene

Hayo ameyasema katika mapokezi ya mbio za Mwenge wa Uhuru katika Halmashauri ya wilaya ya Mpwapwa wenye kauli mbiu “Sensa ni Msingi wa Mpango wa maendeleo. Shiriki kuhesabiwa  tuyafikie maendeleo ya Taifa.”

“Watu wanahitaji kusikia shida zao zinazungumzwa, ni imani yangu kwamba viongozi tutaendelea kushirikiana na fedha yoyote ya mradi wa maendeleo itakayokuja tutaitumia vizuri," amesema Waziri Simbachawene