Akizungumza na www.eatv.tv, Chuchu amesema kitendo cha watu kumtukana na kumkashifu wema kutokana na tatizo hilo halivumiliki, kwani amejaribu kuvaa viatu vyake na kuyajua maumivu yake kama mwanamke.
“Wema ni mtu wangu wa karibu ukiachilia mbali ni mfanyakazi mwenzangu, nikasema nilijaribu kuvaa kiatu cha wema, watu wanajisahau sana, sio kila kitu mtu unaweza ukampiga fimbo, unaweza ukamuathiri kisaikolojia, hao hao baadae watakuja kumcheka, ifike hatua mashabiki wetu tunapopata matatizo wawe wanatupa moyo na sio kutukatisha tamaa, nimeumia sana, yeye ameandika kwa furaha, lakini matokeo yake anasoma coment anakuta zinamuumiza, nikasema acha niwaambie”, amesema Chuchu.
Jambo hili limetokea baada ya Wema Sepetu kumposti mtoto wa Chuchu na Ray kwenye instagram, na ndipo watu wakaanza kumporomoshea matusi wakimkebehi kwa yeye kutofanikiwa kuitwa mama mpaka sasa.


