Jumatano , 25th Mei , 2022

Bodi ya Nyama Tanzania (TMB), imepiga marufuku matumizi ya nondo nyeusi katika maduka ya nyama, na badala yake zitumike nondo za silver ikiwa ni hatua mojawapo ya kuboresha biashara ya nyama katika mkoa wa Kagera.

Nyama zikiwa zimening'inizwa kwenye nondo zilizozuiliwa

Agizo hilo limetolewa na Daktari wa mifugo kutoka TMB ofisi ya Kanda ya Ziwa, Msomi Anthony, wakati wa ukaguzi wa maduka ya nyama na machinjio mbalimbali katika Manispaa ya Bukoba, ambaye amesema kuwa nondo nyeusi zinasababisha nyama kuharibika haraka kutokana na kupata kutu. 

"Tumepiga marufuku matumizi ya nondo nyeusi, lakini pia tumezuia uendeshaji wa biashara bila kufuata utaratibu kwa maana ya uwepo wa wadau ambao hawajasajiliwa, na pia tumefanya kazi ya kuhakikisha unaundwa umoja ili wadau waweze kupata fursa zilizopo katika mnyororo wa thamani wa nyama, tunashukuru Mungu tunakwenda vizuri," amesema Dkt. Anthony