
Mkurugenzi Mtendaji wa WFP, Bi. Ertharin Cousin
Shirika hilo pia limeomba kiasi cha Dola za Marekani milioni 204 (Zaidi ya shilingi bilioni 500 za kitanzania) kwa ajili ya kununua chakula na kukisafirisha kwenda eneo hilo kuwasaidia mamilioni ya watu wanaokabiliwa na njaa.
Mkurugenzi Mtendaji wa WFP, Bi. Ertharin Cousin, amesema janga la El Nino limechochea ukame ambao umeiathiri Amerika ya Kusini na Ethiopia na kusababisha uharibifu wa mazao na mavuno kuporomoka katika nchi za Kusini mwa Afrika huku Malawi ikiathirika zaidi.
Bi. Cousin amesema, kwa sasa watu milioni 18 wanahitaji msaada wa dharura wa chakula katika nchi za Lesotho, Madagascar, Msumbiji, Swaziland, Zambia. Zimbabwe na Malawi.
Amesema, shirika hilo linatarajia kuongezeka kwa mahitaji baada ye mwaka huu na inakadiriwa kwamba watu milioni 33 wataathirika kwa El Nino na janga la La Nina.