Jumatano , 27th Jan , 2016

Shirika la Afya Duniani, WHO limesema kesho litaitisha mkutano maalum kuhusu kirusi aina ya Zika ambapo kirusi hicho tayari kimeripotiwa kwenye nchi 20 huku Brazil ikiwa ni nchi iliyoathirika zaidi.

Msemaji wa WHO Christian Lindmeier

Akizungumza na waandishi wa habari mjini Geneva, Msemaji wa WHO Christian Lindmeier ameeleza kwamba kirusi chenyewe cha Zika si hatari, kwani husababisha ukurutu mwilini.

Hata hivyo ameeleza kwamba Brazil imeshuhudia pia visa 4,000 vya watoto wanaozaliwa na vichwa vidogo, miongoni mwao 49 wakiwa wamefariki dunia, ikidaiwa hali hiyo kuwa na uhusiano na kirusi cha Zika.

Aidha amesema kwamba WHO haijapendekeza wanawake kujikinga dhidi ya kupata mimba, akieleza kwamba suluhu dhidi ya kirusi cha Zika hivi sasa ni kujikinga na mbu aina ya Aedes, ikiwa ni Brazil au kwingineko.