Wizara yaombwa kusimamisha masomo

Jumanne , 17th Mar , 2020

Mtandao wa wanafunzi nchini (TSNP), umeiomba Wizara ya Elimu kutoa tamko la kusimamisha masomo kwa Vyuo, Vyuo Vikuu, Shule za Msingi na Sekondari, ikiwa ni hatua ya kujikinga na athari ya maambukizi ya ugonjwa hatari unaosababishwa na virusi vya Corona.

Waziri wa Elimu, Joyce Ndalichako

Taarifa hiyo imetolewa na Mwenyekiti wa mtandao huo Davis Komba, kwa kile alichokieleza kuwa Serikali inapaswa kuzingatia suala hilo kama ambavyo Mataifa mengine yalivyoamua kufunga shule baada ya kugundua visa vya waathirika wa ugonjwa huo.

"Wizara ya Elimu ione vyema kusimamisha masomo kwa Shule, Vyuo na Vyuo Vikuu kama hatua ya tahadhari kwa umma, kwani wanafunzi wapo kwenye hatari kubwa ya kuambukizwa" imeeleza taarifa hiyo.