Jumamosi , 20th Mei , 2023

Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi zimetia saini hati za makubaliano na Wizara ya Ardhi, Maendeleo ya Makaazi Zanzibar katika ushirikiano kiutendaji na kuweka mifumo madhubuti ya usimamizi katika sekta za Ardhi kwa pande zote mbili

Mbali na hapo Shirika la Nyumba la Tanzania na Shirika la Nyumba la Zanzibar wamekubaliana kutatua changamoto za Ardhi zilizopo ikiwa ni utekelezaji wa agizo la Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan la kuhakikisha changamoto za Muungano zinatatuliwa.

Utiaji huo saini saini umeshuhudiwa na Mawaziri wa Sekta ya Ardhi Tanzania Bara na Visiwani