Alhamisi , 17th Mar , 2016

Zaidi ya watu 40 wanashikiliwa na Jeshi la Polisi visiwani Zanzibar, kwa tuhuma za kuhusishwa na matukio mbalimbali ya uhalifu ikiwemo waliohusika na milipuko ya mabomu katika kisiwa cha Unguja.

Waziri wa Mambo ya Ndani Charles Kitwanga.

Akiongea na Waandishi wa habari jana Visiwani humo Waziri wa Mambo ya Ndani Charles Kitwanga amesema watu hao wanashikiliwa na jeshi la Polisi kwa upelelezi zaidi ili kubaini endapo walihusika katika matukio ya uhalifu visiwani humo.

Aidha Mhe. Charles Kitwanga ametumia fursa hiyo kuwatoa wasiwasiwa Wananchi wa visiwa hivyo na kuwataka kujitokeza kwa wingi siku ya uchaguzi wa marudio unaotarajiwa kufunyika Machi 20 mwaka huu.

Pia Waziri huyo wa Mambo ya Ndani amekanusha taarifa zinazotolewa na baadhi ya vyombo vya habari juu ya watu wanaokimbia visiwa hivyo wakihofia usalama wao na kuainisha kuwa taarifa hizo ni uzushi.