"Zamani ukipiga chafya, unaambiwa afya" - Polepole

Ijumaa , 22nd Mei , 2020

Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Hamphrey Polepole, amesema kuwa chama chake kimekaa na kutafakari kwa muda, kufuatia hofu iliyojengeka kwa wananchi iliyopelekea hata ikifikia hatua ya kupiga chafya, lazima mtu ajifikirie na kumpongeza Rais Magufuli kwa maono yake makubw.

Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Hamphrey Polepole.

Polepole ameyabainisha hayo leo Mei 22, 2020, Jijini Dar es Salaam, wakati akizungumza na waandishi wa Habari katika ofisi za chama hicho zilizopo Lumumba, na kusema kuwa isingekuwa maono ya Rais Magufuli ya kuzuia kila mtu kutoa taarifa za ugonjwa wa Corona, basi hali isingekuwa nzuri.

"Chama kilikaa muda kikatafakari kikasema, hivi si tumekua maisha yetu yote mtu akipiga chafya tunamuambia afya!, leo ukipiga chafya imekuwa ni hukumu unaweza ukachukuliwa hatua, tukaseme tujiongeze tuchukue hatua, na ndiyo maana hata hili jambo la kufungia watu ndani kama mifugo, Mataifa makubwa wananchi wanaandamana" amesema Polepole.