Jumatano , 4th Nov , 2015

Tume ya Uchaguzi Zanzibar ZEC na katibu mkuu wa chama cha wananchi CUF Maalim Seif Sharif Hamad wametakiwa kukaa meza moja na kutafuta muafaka wa tatizo la uchaguzi mkuu linaloendelea kwa sasa visiwani humo.

Naibu Mkurugenzi Utawala, fedha, mipango na utatuzi wa migogoro chuo cha Diplomasia Dkt.Bernard Achiula

Naibu Mkurugenzi utawala, fedha, mipango na utatuzi wa migogoro chuo cha Diplomasia Dkt. Bernard Achiula ameyasema hayo leo jijini Dar es Salaam na kuongeza kuwa kuwa si jambo la kawaida kwa tume hiyo kuahirisha zoezi hilo ghafla bila kumuita mgombea huyo wa nafasi ya urais na kutumia busara ya kumuelekeza taratibu za uchaguzi kwa kile alichokifanya.

Aidha Dkt. Achiula amesema kuwa uamuzi waliouchukua ni sawa na kuwadhulumu wananchi haki yao kikatiba kwa kura walizopiga tarehe 25 Oktoba bila kutangaziwa kiongozi waliyemchagua na ambaye atawaongoza kwa kipindi cha miaka 5 ijayo.

Aidha Dkt. Achiula ameongeza kuwa kitendo cha kujitangazia matokeo bila ruhusa ya ZEC ni makosa kisheria na kikatiba huku akitumia nafasi hiyo kuwaasa wananchi wa visiwani humu kuwa wavumiluvu wakati suala hilo likitafutiwa ufumbuzi.