Alhamisi , 17th Oct , 2019

Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) imeanza kutekeleza agizo la Rais Magufuli, kwa kuwakamata viongozi 50 wakiwemo Wenyeviti, Wajumbe wa Bodi na Makarani vyama (13) vya Msingi na Ushirika (AMCOS) Mkoani Lindi

kwa kutolipa fedha za wakulima zinazotokana na zao la Ufuta Jumla ya Sh Mil.486.

Naibu Mkurugenzi Mkuu wa TAKUKURU, Brigedia JeneralI, John Mbungo ameyaeleza hayo alipokuwa akizungumza na waandishi wa vyombo mbalimbali vya Habari katika Mkoa wa Lindi, ambapo amevitaja vyama hivyo na viwango, Milindimo AMCOS (Sh,90,711,354/-), Mtunao Amcos (Sh,73,715,760/-), Kipelele Amcos (Sh,57,257,280/), Nachiunga Amcos (Sh,10,780,100/-) Chikonji Amcos (Sh,10,325,550), Mnolela Amcos (Sh,3,052,000/-), na Mageuzi Amcos (Sh,2,630,000/-).

Vingine ni Kinjikitile Amcos (Sh,15,100,000/-), Mtama Amcos (Sh,8,523, 830/-) za wakulima wa Ufuta pamoja na Sh,160,000/-) za Chama cha Ushirika Lindi Mwambao, Matumbi Amcos (Sh,12,154,604/-), Mandawa Amcos (Sh,4,095,200/-),Mchinga Amcos (3,604,500/-) na Mmangwa ngwa Amcos (Sh,3,314/-) (Sh,3,314,300).

Naibu Mkurugenzi Mkuu huyo wa TAKUKURU amewataja wanaoshikiliwa na vyama vyao kwenye mabao ni, Mwenyekiti Hemedi Yasini Kilete, Said Hemedi Mkwera, Twahili Kilete, Hillard Cosmas, Chadili na Hassani Lidemu, ni Makarani (Milindimo Amcos), Hassani Liunja na Karimu Nggara, ni makarani (Mtunao Amcos).

Wengine ni Zuberi Omari Nolelei (Mwenyeikti) na Mjamari Haji Kibohu (Katibu) wa {Kipelele Amcos},Said Mohamedi Mbunda (makamu mwenyekiti),Nasra Chigwile (Karani), Mathiuad Mohamedi Likumwili,Chande Mshamu Mandadu na Issa Lutumno (wajumbe) wa Nachiunga Amcos.