Alhamisi , 10th Feb , 2022

Jeshi la Zimamoto na Uokoaji nchini limesema kwamba litaboresha mifumo yake ya kidigitali katika utoaji wa taarifa kwa umma, utakaowezesha kutoa taarifa kwa wananchi wengi kwa wakati mmoja ili kutatua changamoto za majanga ya moto.

Msaidizi Mwandamizi wa Jeshi la Zimamoto Tanzania, Puyo Nzalayaimisi

Kauli hiyo imetolewa na Msaidizi Mwandamizi wa Jeshi la Zimamoto Tanzania Puyo Nzalayaimisi, wakati wa ziara yake ya kutembelea vyombo vya habari vya makampuni ya IPP Media, ambapo aliongozana na maafisa habari wa jeshi hilo kutoka mikoa mbalimbali ya zimamoto mkoani Dar es Salaam.

Kwa upande wake Mkaguzi wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji mkoa wa Ilala Elinimo Shang'a, ameeleza matembezi ya jeshi hilo yatakayowahusisha na wamachinga katika uhamasishaji kwa wananchi kutumia namba ya dharura ya jeshi hilo katika kupata usaidizi pindi majanga yanapotokea.