Mbunge wa Kigoma Mjini, Zitto Kabwe
Zitto amebainisha hayo baada ya kupokea maombi kwa baadhi ya watu mbalimbali wakiwemo viongozi wakubwa wakimtaka akachukue fomu ya Urais TFF pindi dirisha likifunguliwa ili aweze kugombea nafasi hiyo hapo awali.
"Nimetafakari na kuchukua uamuzi kwamba uongozi wa ACT- Wazalendo na Ubunge ni nafasi ambazo ninazo tayari, wakati Urais TFF ni nafasi mpya. Kwa hali hiyo na kwa mapenzi makubwa ya soka la Tanzania, nimeamua nisichukue fomu ya kugombea Urais TFF kwani naweza kuomba kazi ambayo nitashindwa kuitumikia kwa muda wa kutosha kutokana na majukumu yangu kwenye chama na Ubunge" aliandika Zitto kupitia ukurasa wake wa facebook.
Aidha, Zitto ameendelea kwa kusema uamuzi wake umezingatia umezingatia mapenzi makubwa ya kwa soka la Tanzania.
" Nikijitokeza kuwania Urais wa TFF leo halafu nikakosa muda mzuri wa kutimiza matarajio ya wapenda soka nchini, utakuwa ni usaliti mkubwa kwa maendeleo ya soka la Tanzania" alisisitiza Zitto.
Huu ndiyo ujumbe wa Zitto Kabwe kupitia ukurasa wake.