Wanaommendea mume wa Riyama wapewa darasa

Jumamosi , 12th Jan , 2019

Muigizaji anayefanya vizuri kwenye Bongo Movie, Riyama Ally amewapa somo wanawake wenye tabia za kuiba waume za watu wawe wapole na siyo kujitutumua.

Riyama na mume wake siku ya ndoa yao.

Kupitia kipindi cha Friday Night Live, Riyama amesema kwamba katika mahusiano yake na mume wake, Leo Mysterio zipo changamoto nyingi anazopata ikiwepo usumbufu wa wanawake wanaomsumbua mume wake kwa kumtaka kimapenzi.

Ameongeza kwamba hashangai wakimtaka kwa kuwa mwanaume wake ni mzuri lakini wafahamu kwamba ni mume wa mtu hivyo wafanye kwa adabu.

"Usumbufu haukosi. Unaambiwa ukiwa na mwanaume mzuri lazima ugomvi na wanawake wenzako.  Mume wangu ni mzuri Mashallah . Niseme kama unajaribu kuiba kuwa mpole siyo kutaka kujitutumua kama kupiga chafya, ukichonga mdomo, wenzako wanachonga jeneza. Usije kujidai unadanga kumbe unadangiwa"- Riyama.

Akizungumzia kuhusu wasanii wenzake kummendea, Riyama amesema japo hapendi kuwaweka wazi lakini anawafahamu na wafanye ustaarabu kwa kuwa haipendezi.