20% afunguka stori ya Neema na kupata watoto wengi

Jumanne , 19th Mei , 2020

Msanii wa BongoFleva aliyetamba kipindi cha nyuma 20 Percent, amefunguka kusema ile filamu yake ya 20% Furaha Iko Wapi na wimbo wa Mama Neema, ni stori ya kweli japo haimuhusu moja kwa moja.

Msanii mkongwe wa BongoFleva 20 Percent

 

Akipiga stori na Big Chawa kwenye kipindi cha PlanetBongo ya East Africa Radio, msanii huyo ameeleza kuwa,  "Ile ngoma ya Mama Neema ni stori ya ukweli japo hainuhusu mimi moja kwa moja na ilitoka mwaka 2007, Neema sasa hivi ni mkubwa na anajiheshimu pia anasifa kama za Monalisa japo kwa sasa yupo nchini Rwanda, halafu binafsi nimebarikiwa kupata watoto wa kutosha yaani ninao wengi" amesema  20 Percent.

"Nakuja na filamu ya pili ya Mama Neema, itaonesha Neema alivyotoroshwa na mama yake mdogo kwenda Rwanda, kipindi naiachia ile filamu zilivumishwa stori eti nilikataza nyimbo zangu zisipigwe kwenye Media, ndiyo maana nikazihamishia kwenye ile filamu" ameongeza.