Jumatano , 2nd Apr , 2014

20%, msanii wa muziki wa kizazi kipya nchini Tanzania, amesema kuwa kwa sasa amegeukia kwa nguvu zote sanaa ya maigizo ambapo ameweka wazi kuwa anaweka nguvu zake zote katika kukamilisha filamu yake ambayo itatoka hivi karibuni.

20%

20% amesema kuwa, hatua hii ni ambayo itaonyesha upande mwingine wa kipaji chake ni kwa ajili pia ya kujiongezea kipato, ambapo amekiri kuwa sanaa hii ya maigizo ikifanywa vizuri inaweza kulipa zaidi ya watu wengine wanavyofikiri.

Kwa sasa mashabiki wa msanii huyu wanasubiri kwa hamu kubwa kuona ni nini ambacho msanii huyu anaweza kukifanya kwa upande wa uigizaji baada ya mafanikio na hatua kubwa ambazo tayari amekwishapiga kimuziki.

Tags: