"Acha niwe Chawa wa Harmonize" - H Baba

Jumanne , 21st Jul , 2020

Kutokea pande za Mwanza msanii H-Baba amejibu yanayoendelea kwenye Jamhuri ya watu wa mitandaoni, kwamba amekuwa Chawa wa Harmonize kwa kusema, ni vizuri kwa sababu hayo ni maoni ya watu na hatakiwi kuyapinga.

Picha ya pamoja kulia ni H Baba na kushoto Harmonize

Akipiga stori na EATV & EA Radio Digital, amesema acha aendelee kuwa chawa wa Harmonize kama wanavyosema ila yeye atasimama kama H-Baba, kwani hata Harmonize amemkuta hivyo hivyo.

"Ni vizuri sana kwani ni maoni ya watu hutakiwi kuyapinga, mimi ni shabiki namba moja wa Harmonize pili ananiheshimu, acha niwe chawa wa Harmonize kama wao wanavyojua ila mimi nasimama kama H Baba kwa sababu hata Harmonize amenikuta nikiwa hivi, kuitwa Chawa haiwezi kuniathiri japo wanatengeneza hivo hadi kuingilia familia yangu" ameeleza H-Baba.

Zaidi Bonyeza hapa chini kwenye Video