Achukua mkopo kumnunulia gari mpenzi wake

Jumatano , 14th Feb , 2018

Binti mmoja mwenye umri wa miaka 20 wa nchini Kenya, Frida Kariuki, amemzawadia mpenzi wake gari aina ya mercedes, kama zawadi ya valentine hii leo.

Binti huyo ambaye ni mwanafunzi wa chuo kikuu cha Kenya Methodist, amesema pesa ya kununua gari hiyo yenye thamani ya milioni 28 za Kenya, amechukua mkopo kwa baba yake ili mradi amfurahishe mpenzi wake.

Mpenzi wake huyo anayejulikana kwa jina la Mike mwenye umri wa miaka 25, alichukua huku akiwa amemfunga macho kwa kitambaa, ili kumsuprise kwa zawadi hiyo ya aina yake, ambayo kwa maisha ya sasa ni nadra kufanyika.

Haya ndio mahaba niue nichukue mkopo kwa baba!!