Jumanne , 21st Apr , 2015

Rapa Adili Mkwera, aka hisabati au magazijuto amejipanga kusimama kidedea kuuokoa muziki wa hip hop kutokana na kile anachosema kuwa muziki huo kwa sasa haupewi kipaumbele kwenye vyombo mbalimbali vya habari nchini.

msanii wa miondoko ya Hip Hop nchini Adili aka Hisabati

Adili ambaye ni mmiliki wa studio ya chapakazi mkoani Mbeya ameelezea kuwa studio yake hiyo imejipanga kuanza matayarisho makubwa ya kuandaa show itakayokuwa mahususi kwa ajili ya kuinua aina ya muziki huo.

Aidha rapa huyo wa studio hiyo ya chapakazi ambaye licha ya kuwa promota na mtayarishaji mkuu wa studio hiyo amesema kuwa huu ni mwaka wa kuanza kuirudisha hip hop katika chati.