
Akizungumza kwenye Planet Bongo ya East Africa Radio alipokuwa akifanya mapitio ya albam yake 'Money Monday', Vanessa amesema anaelewa Afande Sele ni mkongwe kwenye game, na huenda alikuwa na stress zake binafsi hivyo alikuwa anatafuta wa kummalizia hizo hasira, na ndipo alipoangukia kumponda Vanessa Mdee.
Mi nilimuelewa, niliangalia anazungumzia kwa upande gani, nikagundua in few seconds nimetumika kama 'punching bag', sikuchukulia personaly nikaona fresh kabisa, nikajua ah na yeye anataka kusikika anatafuta pa kutokea kiivyo, halafu mimi ni shabiki yake mkubwa ila akawa kama ameniua, amenitathmini, akaona vile, ila ukweli yule ni legend pia”, amesema Vanessa Mdee.
Licha ya hayo Vanessa Mdee amesema hajaacha kuwa shabiki wa Afande Sele kwani anakubali kazi zake, huku akisema kitendo cha Afande kusema anabebwa hakina ukweli kwani yeye ni miononi mwa wasanii wanaopigana sana kwenye kazi zao.