
Afande Sele
Akizungumza na mwandishi wa East Africa Radio, Afande Sele amesema kitendo cha vijana hao kulelewa kuna wapa madhara makubwa ikiwemo kuwa watumwa katika mapenzi, na matokeo yake kuishiwa nguvu za kiume na kununua dawa za kuongeza nguvu hizo, ili waweze kupambana na hali hiyo.
"Mimi nadhani tabia hiyo ya vijana kupenda kulelewa inawanyima uhuru binafsi kwa sababu unapokuwa unaishi na mtu ambaye kila kitu chako unamtegemea yeye inamaana uhuru wako wa maisha ameushika, lakini pia uwezo wako wa kufikiri unapungua kutokana unajikuta muda mwingi unafikiria kumfurahisha mtu mwingine, ndiyo maana unaweza kuta hata mapenzi hujisikii na kitendo hicho kinasababisha kwa asilimia kubwa kwa kukosa nguvu za kiume na matokeo yake inapelekea kununua dawa za kuongeza nguvu za kiume 'Viagra'', alisema Afande Sele.
Msikilize hapa chini