
Msanii Official Agness
Akizungumza kwenye kipindi cha MamaMia ya East Africa Radio wakati anatoa mchanganuo wa mahari hiyo Official Agness ameeleza kuwa
"Bila milioni 500 hakuna ndoa, kuna gharama nyingi zimetumika kwa wazazi wangu kama shule, chuo hata mimi nimetumia gharama nyingi kufika hapa pia ni mpambanaji pia, akitokea mtu akanilipia Milioni 500 atakuwa ananipenda sana”
"Nimeamua kujipa thamani wazazi wangu wamepambana sana, kwahiyo siwezi kuolewa kwa gharama ndogo ya Milioni 2 au Milioni 3" amesema Official Agness
Aidha ameendelea kusema wazee wa zamani walidumu kwenye ndoa kwa sababu pesa haikuwa na thamani kwao lakini sasa hivi pesa ndiyo kila kitu kwenye ndoa.