
Akiongea kwenye kipindi cha Planet Bongo cha East Africa Radio, Ben Pol amesema albamu hiyo itakuwa na kollabo za wasanii mbalimbali, kutoka Tanzania, Kenya na Nigeria.
“Album ipo hatua za mwisho tayari kuna nyimbo tisa zimeisha, tunasubiria Mwana FA aingize, hapa bongo kutakuwa na Baraka, Ngosha (Fid Q) Afrika tuna Nameless, tuna Avril, Bank W wa Nigeria, pamoja na Chidinma kuna wimbo ambao tunafanyanae hajamaliza bado,” alisema Ben Pol.
Ben Pol ambaye kwa sasa ana kazi mpya hewani ya 'Moyo mashine', ametumia pia fursa hiyo kumshukuru Prodyuza Loli Pop, kwa kazi kubwa aliyoifanya kwenye wimbo huo ambao umekuwa gumzo kwa mashabiki.