Alikiba
Muda mfupi baada ya kuachia wimbo huo, Alikiba ameeleza siri nzito iliyopelekea kuachia wimbo huo hivi sasa.
Katika ukurasa wake wa Twitter, Alikiba amesema kuwa wimbo huo aliuandika takribani miaka 10 iliyopita aliposafiri kwa mara ya kwanza nchini Oman.
Mara ya mwisho kwa Alikiba kutoa wimbo wa peke yake ni takribani miezi minne iliyopita ambapo alitoa wimbo wa Kadogo.