Jumatatu , 17th Jun , 2019

Msanii wa Bongofleva Alikiba, amefanya mazungumzo na balozi wa Ufaransa Frederic Clavier leo Juni 17, 2019, ambapo wamekubaliana mambo mbalimbali ikiwemo kuendelea kubadilishana utamaduni.

Alikiba akiwa na Balozi wa Ufaransa Frederic Clavier

Alikiba amethibitisha mchongo huo leo kupitia ukurasa wake wa mtandao wa Instgram ambapo amendika, ''Mapema asubuhi ya leo nilipata fursa ya kufanya mazungumzo na Balozi wa Ufaransa nchini - His excellence Frederic Clavier ofisini kwake''.

Akiweka wazi mazungumzo yao, amefunguka haya, ''Tumezungumza mengi kuhusu namna gani tunaweza kujenga daraja la kubadilishana utamaduni baina ya Tanzania na Ufaransa''.

Alikiba ni miongoni mwa wasanii ambao huenda wakawa wanafahamu kidogo lugha ya Kifaransa ambapo amewahi kuimba baadhi ya mashairi yake kwa Kifaransa katika wimbo wake wa Aje.