Jumatatu , 3rd Dec , 2018

Mkali wa Bongofleva ambaye kwasasa ametambulisha 'Label' yake ya muziki inayofahamika kama (Kings Music Record Label) ambayo ina wasanii wanne, ametoa sharti dogo kwa wapenzi wa muziki wake kama wanataka ngoma mpya kutoka kwake.

Msanii Alikiba

Kupitia ukurasa wake wa Instagram Alikiba ametoa mkwara huo kwa kuwaaambia mashabiki kuwa ngoma mpya ya wasanii wa Kings Music iitwayo 'Toto' ni kali na kwa anayebisha amemtaka akune kichwa ili aachie ngoma.

''TOTO ni shida fanya kama unajikuna nitoe kubwa'', umesomeka ujumbe huo kutoka kwake.

Katika ngoma hiyo ambayo imeachiwa wikiendi iliyopita, Alikiba hajaimba kama alivyofanya kwenye wimbo wa kwanza badala yake amewaacha wasanii Abdukiba, Cheed, Killy na K-2GA.

Alikiba hajatoa wimbo wa peke yake tangu Mei 11, 2018 alipoachia Mvumo wa Radi, lakini alishirikiana na wasanii wa Kings Music kwenye wimbo wao wa kwanza ulioitambulisha Lebo hiyo uitwao 'Sina'.