Jumanne , 19th Mar , 2019

Msanii wa kizazi kipya asiyekaukiwa na vituko mjini, Amber Lulu anadaiwa kumpora mpenzi wa msanii mwenzake anayejulikana kwa jina la Haitham Kim.

Amber Lulu

Stori za Amber Lulu kumpokonya Haitham mpenzi ambaye pia ni mzazi mwenzake, zilianzia kwenye mitandao ya kijamii baada ya msanii huyo ku-post picha ya kaka huyo na kisha kuweka alama ya makopa kopa.

Kama hiyo haitoshi, Amber Lulu aliweka maneno yenye utata kwenye ukurasa wake wa Instagram akirusha jiwe gizani ambalo limetafsiriwa kuwa ni dongo la msanii mwenzake.

"Ungetaka awe wa kwako peke ako ungemzaa wewe,  kwani si atuna macho, sirembii", ameandika Amber Lulu.

Hata hivyo baada ya ujumbe huo Haitham katika ukurasa wake aliweka picha ya ua jeusi na ujumbe wenye kuashiria kuvunjika kwa mahusiano yake na Baba wa mtoto wake.

Pamoja na hayo, katika kuonyesha ugomvi anauweza Amber Lulu akampost mwanaume huyo kwa maneno kwamba,"mwendo wa kuenjoy  miluzii kidogo".

Katika kutaka kuthibitisha tuhuma hizo kama zina ukweli, Amber hakupatikana katika simu yake ya mkononi huku Haitham Kim simu yake ikiwa hapokelewi.