Jumanne , 22nd Oct , 2019

Video Vixen na msanii Amber Rutty, ametangaza kuwa tangu ameolewa na mume wake Davil, hajawahi kuvaa nguo za ndani akidai kuwa zinambana na anaogopa joto la Dar Es Salaam, ambalo litasababisha uvundo kwenye nguo hizo.

Akieleza hayo kupitia EATV & EA Radio Digital, Amber Rutty amesema, huwa anapenda kuongea ukweli na kwenye hilo ana asilimia kubwa kuwa hajawahi kuvaa nguo za ndani.

"Sitaki kuongea uongo na ukiongea unafiki haileti picha nzuri kwenye jamii, napenda kuongea ukweli ili hata watu wajifunze wasiwe wanaongea uongo, asilimia kubwa mimi binafsi tangu nimeolewa sijawahi kuvaa nguo za ndani, kwanza inanibana pili itatoa uvundo kwa joto hili la Dar Es Salaam na kushindwa kupata hewa, nina nguo za ndani mbili kwa ajili ya 'Period' tu hizo zingine sina" amesema Amber Rutty.

Amber Rutty ameendelea kusema, hawezi kuweka nguo za ndani nyumbani kwake wakati anajua hazitumii, mwisho wa siku zije kuwa takataka na uchafu.

Aidha amewasema Wanawake ambao wanatabia ya kutembea na nguo za ndani kwa kusema.

 "wanajidanganya kwa wanaotembea na nguo za ndani kwa sababu huwa wanavaa kisha wanaziweka kwenye sehemu ya kutupia taka hadi zingine kuliwa na panya na kujaza uchafu ndani"