Ijumaa , 26th Jan , 2018

Msanii mkongwe wa bongo fleva Ismael maarufu kama Voice Wonder ambae alifanya vizuri na wimbo wake wa 'nimpende nani' hapo zamani amefunguka kwa kumwagia sifa Aslay kuwa ndio mtu ambaye anamkubali kwa jinsi anavyofanya kazi zake.

Msanii Aslay

Voice Wonder ameeleza hayo kupitia Heshima ya Bongo Fleva inayorushwa mubashara EATV kutoka kwenye kipindi cha Planet Bongo ya 'East Afrika Radio' na kusema wapo wengi wanaofanya vizuri lakini kwa sasa huyo ndie anayemvutia.

"Watu wanaofanya muziki mzuri ni wengi sana lakini katika wasanii wa sasa napenda sana anavyofanya kazi Aslay", alisema Voice Wonder.

Voice Wonder

Kwa upande mwingine, Voice Wonder amesema amerudi rasmi katika muziki huku akiwataka mashabiki zake kumpa ushirikiano katika ujio wake mpya ambao anatarajia kuachia ngoma yake ya kwanza baada ya wiki mbili kutoka sasa ambayo atakuwa amemshirikisha Barnaba.