Jumanne , 19th Aug , 2014

Mwanamitindo Ataui Deng ambaye alipotea kwa muda wa siku 10 huko jijini New York nchini Marekani, hatimaye amepatikana akiwa hai, mpango uliofanikiwa baada ya kampeni kubwa ya kumsaka iliyoendeshwa na mwanamuziki nyota Rihanna.

mwanamitindo kutoka nchini Sudan Ataui Deng

Mwanamitindo huyu ambaye ana rekodi kubwa katika fani hiyo, amepatikana katika eneo karibu na Hospitali huko Manhattan.

Taarifa za kupotea kwa Ataui ambaye asili yake ni nchini Sudan, zilitolewa na Polisi na kuzua hofu kubwa huko New York ambapo amekuwa akiishi toka mwaka 2008 akifanya shughuli zake za mitindo.