Jumatano , 27th Mei , 2026

Msanii wa muziki kutoka Nigeria Ayra Starr ameendelea kuonyesha kuvutiwa kwake na kufanya kazi na staa mwenzake Burna Boy, huku jina la Burna likitajwa mara nyingi zaidi na Ayra ukilinganisha na wasanii wengine wengi wa ndani na nje ya Nigeria.

Pichani ni Burna Boy na Ayra Starr

Kwa mujibu wa mahojiano mbalimbali aliyofanya katika kipindi cha zaidi ya miaka mitatu mfululizo, Ayra Starr amekuwa akimtaja Burna Boy kama msanii ambaye anatamani zaidi kufanya naye collaboration, akifuatiwa na superstar wa Marekani Rihanna.

 

Katika zaidi ya interview tano tofauti, Ayra amesisitiza kuvutiwa kwake na ubunifu pamoja na mchango mkubwa wa Burna Boy kwenye muziki wa Afrika, jambo ambalo limeendelea kuwapa matumaini mashabiki kuhusu uwezekano wa wasanii hao kufanya kazi pamoja siku zijazo.

 

Hadi sasa bado hakuna taarifa rasmi kuhusu uwepo wa collabo kati ya Ayra Starr na Burna Boy, lakini mashabiki wengi wanaamini huenda ushirikiano huo ukatokea muda wowote kutokana na namna Ayra anavyoendelea kuonyesha hamu ya kufanya kazi na staa huyo wa Afro-Fusion.