Baada ya Vanessa,mwingine atangaza kustaafu muziki

Alhamisi , 25th Jun , 2020

DJ, Muandishi wa nyimbo na mtayarishaji wa muziki nchini Marekani Dj Khaled (45) ametangaza nia ya kustaafu kufanya shughuli zamuziki huku akitaka kuwa kama Jay Z  au Michael Jordan kwenye upande wa mchezo wa NBA.

Mtayarishaji wa muziki Marekani Dj Khaled

Akitangaza nia hiyo kupitia mtandao wa kijamii wa Instagram Dj Khaled ameeleza kuwa "Ningeweza kustaafu kama walivyofanya Jay Z na Michael Jordan walivyofanya muda wowote ambao ningetaka, naweza kustaafu leo na kufurahia yale yote niliyoyatimiza na kuendelea kupokea baraka na upendo zaidi

"Nina shauku ya kushea baraka nyingi, kushawishi na kuwahamisha vijana wengie kwenye ulimwenguni kote, najihisi kama Jay Z na Michael Jordan" ameongeza 

Dj Khaled alianza kazi ya muziki rasmi mwaka 2006 baada ya kuachia Album yake ya kwanza na amefanya kazi na wasanii wakubwa Marekani na duniani kwa ujumla kama Birdman, Lil Wayne, Jay Z , Drake, Nick Minaj, Rihanna , Chris Brown, Justin Bieber, Quavo, Meek Mill, Cardi B na wengineo.