Baba Levo awakataa watoto wake, ataka DNA

Jumanne , 30th Jun , 2020

Msanii na aliyekuwa Diwani wa Mwanga Kaskazini Kigoma Ujiji, kupitia chama cha ACT Wazalendo Baba Levo, amesema ana watoto wengi hadi wengine amewakataa kwa sababu mama zao walikuwa hawajatulia pia ana mpango wa kwenda kuwapima DNA.

Msanii na Diwani Baba Levo

Akipiga stori na Big Chawa kupitia kipindi cha Planet Bongo ya East Africa Radio, Baba Levo amesema yeye ni baba bora kwa watoto wake ila kwenye suala hilo anahitaji vipimo vya DNA ili kuthibitisha.

"Napenda sana watoto japokuwa nina watoto wengi, lakini wengine nimewaweka pembeni kwa sababu wakati natafuta hiyo mimba mama zao walikuwa hawajutulia, walikuwa wana rukaruka leo katembea na huyu kesho katembea na yule, halafu akipata mimba anakwambia ya kwako, kwahiyo mpaka nikawapime DNA nitawachukua na mchakato utaanza baada ya kumaliza kampeni".