Jumanne , 5th Aug , 2014

Akiwa anafanya vyema na wimbo wake uliotokea kutamba katika vituo vya redio nchini Tanzania 'Nani kama Mama', mwanamuziki nyota nchini Christian Bella amepanga kufanya uzinduzi wa wimbo huo mpya.

mwanamuziki Christian Bella wa Tanzania

Christian Bella amesema kuwa atauzindua wimbo huo pamoja na kuuperform kwa mara ya kwanza mbele ya mashabiki wake katika show kubwa aliyoibatiza jina la 'USIKU WA MAMA' itakayofanyika tarehe 29 mwezi huu wa Agosti jijini Dar es Salaam.

'USIKU WA MAMA' itasindikizwa na wasanii Ommy Dimpoz, Matonya, Kassim Mganga, Dully Sykes na bendi maarufu ya Malaika, ambapo pia ataizindua album yake mpya ya Volume 1 itakayosheheni nyimbo sita na video sita.

Bella amesisitiza kuwa wimbo huo ni rasmi kwa ajili ya heshima kubwa kwa akina mama kwani wao ndio waathirika wakubwa wa unyanyasaji duniani.