Isabella kumchukua Jux?

Jumatatu , 8th Apr , 2019

Msanii wa muziki wa Bongo Fleva Isabella Mpanda, ameibua mtafaruku kwenye mtandao wa Instagram baada ya kuonekana kutaka kuchukua nafasi ya Vanessa Mdee kwa Jux, kwa kupost picha yao ya pamoja huku akiandika ujumbe wenye utata.

Picha hiyo ambayo ilipostiwa na Isabella kwenye ukurasa wake wa instagram akiwa na Jux, aliandika ujumbe ambao ulikuwa ukihoji juu ya uwezo wa Vanessa kummudu Jux, huku akiwatolea maneno makali mashabiki wa Vanessa mdee.

Isabella ameandika haya

“Nyie team Vanessa mnikome, huyo boss wenu ana viuno vya kimakonde!?, niacheni nipone, mimi naitwa pipi ya kusini”, aliandika Isabella chini ya picha hiyo.

Hata hivyo haijulikani kama wawili hao ni wapenzi kweli au la, hiyo ni baada ya kuwepo hali ya sintofahamu juu ya mahusiano ya Jux na Vanessa Mdee, kutokana na kuwapo kwa tetesi za wawili hao  kuachana.

Alichopost Isabella kuhusu Jux