Jumanne , 14th Apr , 2026

Mshambuliaji wa Simba, Jonathan Sowah, ameamua kuweka wazi kinachoendelea baada ya kusambaa kwa taarifa kuwa amefungiwa klabuni hapo

Jonathan Sowah,

Katika mazungumzo yake, Sowah amejitetea kuhusu tuhuma za utovu wa nidhamu akisema kuwa yeye ni binadamu na ana pande mbili:

"Watu hawatanipata nikiwa huko nje na uniambie huyu hana nidhamu. Hapana. Wakati wowote utakaonipata kusema sina nidhamu ni uwanjani... Ninapocheza mpira na nikipoteza, nakasirika sana. Lengo langu ni kufunga bao, hata kama nitapata kadi nyekundu au njano, sijali."

Mshambuliaji huyo amewafananisha baadhi ya watu na wachezaji wakubwa duniani kama Mario Balotelli na Diego Costa akieleza kuwa hasira zake ni sehemu ya ushindani wa soka.

Sowa amewatoa hofu mashabiki wa Klabu ya Simba akiwaambia wasiwe na wasiwasi kwani bado ni mchezaji wa Simba na kila kitu kitakuwa sawa