Jumanne , 27th Jan , 2015

Msanii wa muziki Christian Bella amesema kuwa, changamoto ya kuoneana wivu hasa katika bendi za muziki ni kitu cha kawaida, huku akisema kuwa uwezo ndio kitu cha pekee ambacho kinamsaidia kuendelea kubaki juu.

Msanii wa muziki wa dansi nchini Tanzania Christian Bella

Bella ambaye binafsi anajiita 'Sterling', amesema kuwa ni dhahiri kuwa uwezo alionao unazidi wasanii anaofanya kazi nao, na mara nyingi katika kazi huwaachia muda mwingi jukwaani kutoa nafasi kwao pia kujitangaza.