Jumanne , 16th Feb , 2016

Mkali wa Muziki wa R&B Bongo Ben Pol amfunguka kuhusu hali ya mahusiano yake na aliyekuwa Miss Tanzania Namba 2, 2013 Latipha Mohammed.

BEN POL NA LATIFA

Ben Pol amesema ameamua kufunika mahusiano yake kuwa siri na kuamua kuweka juhudi zaidi katika muziki wake.

Ben amesema "sitojishughulisha kutangaza mahusiano yangu ila ikitokea watu wamefahamu basi ni poa. Lakini juhudi zangu zitakuwa kwenye kuutangaza muziki wangu. Hata hivyo kinachoendelea kati yetu ni vya kheri tu na hakuna tatizo".

Hivi karibuni Ben Pol na Latipha waliacha tabia yao ya kupost picha katika mitandao ya kijamii na kupelekea maswali mengi kuwa yawezekana wamemwagana.