Alhamisi , 30th Oct , 2014

Aliyekuwa msanii mahiri wa filamu nchini, Mzee Manento ambaye alijijengea umaarufu mkubwa kupitia kazi maarufu kama vile Dar To Lagos na Fake Pastors, amefariki dunia.

Marehemu Mzee Manento

Kifo cha msanii huyu kimetokea siku ya jana na mpaka sasa msiba unaendelea nyumbani kwa marehemu huko Kigogo jijini Dar es Salaam, na kwa taarifa zaidi juu ya msiba huu, anaeleza hapa Rais wa Shirikisho la Filamu Tanzania, Simon Mwakifambwa.