Jumapili , 1st Mar , 2015

Msanii wa kizazi Kipya nchini Tanzania anayetamba na nyimbo za Mahaba Cassim Mganga amewataka wasanii kutokata tamaa katika maisha hasa katika kupigania muziki kwa kazi ya kumuingizia kipato.

Kassim Mganga

Cassim amesema katika maisha changamoto ni lazima hivyo kama binadamu hutakiwi kukata tamaa mpaka ujue mwisho wake na na kuziona changamoto kama chachu ya kuweza kufika mbali zaidi unapohitaji.

Cassim amesema katika maisha yake hafikirii kukata tamaa kiasi cha kuacha muziki labda muziki umuache yeye huku akisema siyo katika muziki tu hata maisha ya kawaida mwanadamu hutakiwi kukata tamaa.