Jumamosi , 16th Mei , 2015

Chegge, ambaye hivi sasa anabang na project yake mpya kabisa inayokwenda kwa jina Mwananyamala, ameieleza eNewz kuwa mbali na ubora wa video hiyo, tofauti na video zake nyingine amejikita zaidi katika kusimulia kisa cha kile alichokiimba.

Chegge

Staa huyo kutoka TMK Wanaume Family, baada ya kuitambulisha rasmi video ya kazi hiyo jana kupitia FNL amesema kuwa amefurahishwa na mapokezi mazuri ya kazi hiyo ambayo mtazamaji anaweza kuifurahia, na kupata ujumbe wake hata bila kuitazama kwa sauti.

Staa huyo amesema kuwa amefurahishwa na maoni na mapokezi mazuri kabisa ya kazi hiyo ikiwa ni kipindi kifupi tu kutoka kutambulishwa kwake.