Jumanne , 22nd Jan , 2019

Msanii wa muziki nchini Marekani, Chris Brown na wenzake wawili wamekamatwa na polisi wakituhumiwa kwa makosa ya ubakaji.

Tukio hilo limetokea mchana huu Jijini Paris, Ufaransa, baada ya kuwa kwenye uchunguzi wa tuhuma za kudaiwa kumbaka binti wa miaka 24 ambaye alikutana naye katika maeneo ya starehe ya usiku, Januari 15.

Mwanamke huyo alimfungulia mashtaka Chris Brown akilalamika kumfanyia kitendo hicho cha kikatili, alipomualika chumbani kwake akiwa na mwanamke mwenzake, lakini alipokuwa akitoa maelezo yake alienda mwenyewe chumbani na kukutwa na tukio hilo.

Pia mwanamke huyo aliieleza polisi ya Ufaransa kuwa hata walinzi wa msanii huyo mwenye kipaji cha aina yake walimnyanyasa, na ndipo polisi ikaanzisha uchunguzi juu ya tuhuma hizo.

Hata hivyo polisi nchini Ufaransa iliamua kumuachia Chris Brown bila kumfungulia mashtaka, ingawa bado inaendelea na uchunguzi wa tuhuma hizo. 

Baada ya kuachiwa kwake Chris Brown aliandika ujumbe kwenye ukurasa wake wa instagram, kuwa tuhuma hizo hazina ukweli wowote, na kwamba mwanamke huyo alidanganya. 

 I WANNA MAKE IT PERFECTLY CLEAR...... THIS IS FALSE AND A WHOLE LOT OF CAP! NNNNNNNNEEEEEEEEEEVVVVVVVVVVEEEEEERRRRRR!!!!!! FOR MY DAUGHTER AND MY FAMILY THIS IS SO DISPRESPECTFUL AND IS AGAINST MY CHARACTER AND MORALS!!!!!

 

A post shared by CHRIS BROWN (@chrisbrownofficial) on