Ijumaa , 5th Dec , 2014

Mwimbaji nyota wa miondoko ya dansi nchini ambaye pia ni kiongozi na mmiliki wa bendi maarufu ya Malaika Christian Bella hivi sasa amerejea nchini akitokea Sweden kwa ajili ya kufanya ziara zake za muziki nchini ikiwa ni kutambulisha wimbo wake mpya.

Msanii wa muziki wa dansi nchini Christian Bella

Bella ambaye anatikisa na wimbo wake unaofanya vizuri Afrika Mashariki wa Nani Kama Mama ambao alishirikiana na msanii Ommy dimpoz ameongea na Enewz kuhusu safari yake ya kimuziki nchini Sweden, Norway, Oslo, Holland huku akiweka wazi mipango yake ya sasa ikiwa ni kutambulisha wimbo wake mpya akiambatana na bendi yake ya Malaika leo jijini Dar es Salaam.