Jumatano , 16th Oct , 2019

Rapa Country Boy amepiga stori na EATV & EA Radio Digital, na amefunguka kuwa hajawahi kuachwa katika mapenzi na kwamba baada ya kushindwana kitabia yeye na Mama wa mtoto wake waliamua kutengana.

Rapa Country Boy

Akizungumzia suala la kuachana na mzazi mwenziye, Country Boy, amesema kwa sasa ana mtoto wa kiume ila anaishi kwa mama yake, baada ya kutengana kwa kuwa walishindwana ila hakuachwa,

"Nina mtoto nadhani anaenda miaka mitano, lakini Mama yake tulishaachana, sikupenda na sikutaka kuweka mahusiano yangu hadharani kila mtu anaona kwa jicho lake kwa hiyo huenda akaona njia yangu sio sahihi na yeye akaamua kwenda kwa njia yake na tulishindwana ila sijawahi kuachwa kabisa " amesema Country Boy.

Aidha Country Boy amefunguka kuhusu mahusiano ya Officiall Nai na Moni Centrozone, baada ya kusambaa kwa picha katika mtandao wa kijamii wa Instagram ikiashiria kama wameachana.

"Ni mambo tu ya mitandao tu sina uhakika na hilo maana mimi ni mtu wao wa karibu na kama taarifa za kuachana zingekuwa rasmi ningekuwa wa kwanza hata ile picha imefutwa huenda walikwazana maana kwenye mahusiano kuna kugombana na hasira" ameeleza.

Pia amesema watu wasiingilie mapenzi ya watu maana wagombanao ndiyo wapatanao.