
Dan Flavour akiwa katika pozi
Dan Flevor amesema kuwa, hakutaka kuwapatia mashabiki wake taarifa hizi mpaka pale ambapo kazi yenyewe itakuwa imekamilika, ila ameona kuwa ni muhimu kuwatayarisha kwa taarifa za ujio wa kazi hii kubwa.
Kazi hii ni moja ya hatua kubwa kwa msanii huyu ambaye ana matumaini makubwa ya kuongeza mashabiki nje ya mipaka ya Uganda pindi kolabo hii itakapotoka rasmi.