Jumatano , 13th Jul , 2016

Mashindano yanayoendeshwa na kituo cha utangazaji cha EATV yanayokwenda kwa jina la DANCE 100% yanatarajia kuanza kwa kishindo kikubwa siku ya Jumamosi tarehe 16 Julai 2016 katika viwanja vya Leaders Club DSM kuanzia saa nne asubuhi.

Event Coodinator wa shindano hilo Bhoke Egina amesema kwamba shindano la mwaka huu mchujo wa kwanza unatarajiwa kufanyika jumamosi ambapo makundi matano yatapatikana , na tarehe 23 Julai makundi mengine matano yatapatikana na tarehe 30 Julai makundi mengine matano yatapatikana ambapo hapo itakuwa ndiyo mwisho wa usaili.

Baada ya hapo makundi yatachuana katika hatua ya robo fainali na shindalo litaendelea hadi atakapopatikana mshindi na habari kuhusu shindano hili zitakuwa zinatolewa kila wakati na kila baada ya mchujo.

''Tunategemea mwaka huu mashindano yatakuwa na ushindani mkubwa zaidi na usaili wa Jumamosi utashirikisha makundi mengi. Vijana jitokezeni kwa wingi kushiriki pia wasioshiriki kuangalia vipaji vitakavyokuwa vinaoneshwa na vijana wenzao,”Amesema Event Coordinator Bhoke Egina

Aidha vijana ambao wanaruhusiwa kushiriki katika shindano hili ni kuanzia miaka 18 na kuendelea na kwa wenye umri chuini ya hapo , wanatakiwa kuwa na kibali cha wazazi au walezi.

Shindano la mwaka huu zawadi itaongezeka kwa washindi kwa kuwa shindano linadhaminiwa vyema na Kampuni ya vinywaji baridi ya CocaCola pamoja na Kampuni ya simu za mkononi ya Vodacom.

Mwaka huu ni mwaka wa tano wa shindano hili ambapo vijana wengi wamekuwa wakinufaika kuonyesha vipaji vyao na zawadi ambazo hupewa huwasaidia kujiajiri na wengine huweza kunufaika kwa kupendwa na wenye bendi pamoja na wanamuziki binafsi kufanya nao kazi.

Mwaka huu majaji wa shindano hili mwaka huu 2016 ni Super Nyamwela, Lotus Kyamba na Khalila Mbowe upande wa host anasimamia show T- Bway 360 nyote mnakaribishwa.

Tags: