Jumamosi , 1st Aug , 2015

Lile mbilinge mbilinge la Dance 100% limeendelea leo kwa kufanyika usaili wa pili wa mashindano makubwa kabisa ya kudansi nchini Dance 100% 2015 ambao leo makundi kadhaa yamechuana vilivyo katika viwanja vya Don Bosco Upanga.

Moja ya makundi, Mavuno Crew wakionyesha uwezo wao mbele ya majaji katika michuano ya usahili wa pili leo

Timu nzito kutoka EATV na East Africa Radio, Dulla, Dj Summer, Dj Ommy Crazy, Dj Sinorita, T Bay 360, Maggie Vampire na Majaji Super Nyamwela, Queen Darleen na Shetta wamepata kazi kubwa kuyachagua makundi yalichuana vikali

Hakuna kiingilio chochote katika mashindano haya, kwa washiriki wa makundi ya kudansi na hata kwa mashuhuda wa usaili, baada ya kupatikana makundi yanayohitajika sasa ni mbio za kuelekea mchuano mkali wa kumpta mshindi wa Dance Mia mia 2015.... Ivoooooo!!!