Jumamosi , 29th Aug , 2015

Mashindano ya Dance 100% 2015 hatua ya Robo Fainali yanapamba moto leo hii kuanzia wakati huu katika viwanja vya Don Bosco Oysterbay ambapo makundi 15 yaliyofanikiwa kuingia hatua hiyo yatachuana kupata nafasi 10 za hatua ya nusu fainali.

Jukwaa la Dance 100%

Tayari watu wamekwishaanza kumiminika kushuhudia mpambano, Dj Ommy Carazy akiwa anakiwasha katika mashine, Mamie Baby akiamisha kwa stage, kukiwa pia na timu nzima ya east Africa Radio na East AfricaTV kusimamia kila kitu kiende sawasawa.

Itakuwa ni vuta nikuvute kati ya The WD, The WT, Team Makorokocho, Team ya Shamba, Best Boys Kaka Zao, The Winners Crew, Mad Squad, The Heroes Crew, Mavuno Crew, Dream Team, Wazawa Crew, The Best, Cute Babies, Quality Boys na Majokeri ambao kwa wiki nzima umewasikia kila mmoja akijinadi kuchukua ushindi.

Mpambano umeanza kuanzia saa 6 mchana, ambapo burudani hiyo itaambatana na muziki mnene kutoka kwa MaDJS wakali East Africa Radio na vilevile mashindano na zawadi mbalimbali kwa mashabiki kutoka kwa waratibu EATV na pia wadhamini Vodacom Tanzania na Coca Cola ambao ni kinywaji rasmi cha michuano hiyo kwa mwaka huu. Itakuwa ni mafuriko pale Don Bosco, hapo kesho katika Dance 100% 2015.